Nani Anyeiongoza CBC?

Juni 18, 2015

Hatimaye imedhihirika kwamba hakuna mtu yeyote anayeonekana kuiongoza Benki Kuu ya Cyprus (CBC) kuhusiana na suala la FBME tawi la Cyprus. Naam, ni kwenye nafasi ya mwandamizi.

Mamlaka ya Azimio ingeweza kusambaratika kwa hatua zilizochukuliwa dhidi ya FBME Julai iliyopita ambapo haikuonekana kuhusisha Mamlaka kwa ujumla (tazama barua ya Stavros Zenios ‘ya kujiuzulu kutoka bodi ya wakurugenzi ya CBC). Kisha kujiuzulu kwa mkurugenzi mtendaji wa CBC, Stelios Kiliaris, mwezi Machi kumepunguza kamati ya Azimio ya watu watatu hadi wawili, mmoja wao ni Gavana ambaye ni bata anayechechemea baada ya kufanyiwa uchunguzi mkubwa na kamati ya Bunge na polisi.

Hii inabakiza kitengo tu cha Mamlaka, kinachoongozwa na mtu mmoja, Michalis Stylianou, afisa wa ngazo ya chini wa CBC ambaye, inasemekana ameonyesha kujenga uadui wa binafsi na FBME kitambo sasa. Hakika, kwa manufaa ya kila mmoja, siyo yeye anayeongoza kwa sasa wakati viongozi waandamizi wakijihusisha na matukio mengine! Stylianou ndiye ambaye alionyesha kiburi kwa msimamizi mwandamizi kutoka Benki Kuu ya Tanzania. Inajulikana kuwa ndiye aliyekuwa mtawala wa Msimamizi aliyepita, Dinos Christofides lakini inadhaniwa kwamba mtu mwenye busara zaidi Andrew Andronikou angeweza kutambua nia yake.

 Baada ya kusema hayo, Andronikou anahitaji kuwepo Cyprus mara nyingi zaidi kama anataka kujua uwezo wa watu ambao wanamwakilisha ‘mteja’ wake. Kwa sasa anafanya kazi kwa siku mbili au tatu kwa wiki ndani ya FBME tawi la Cyprus na anatuhumiwa kutumia muda wake uliobaki nchini Uingereza. Si mbaya kama unapata EUR 50,000 kwa mwezi. Hata hivyo, kusafiri mara kwa mara kwenda London kunaiweka mashakani ile asilimia 10 ya kikomo cha matumizi walichokubaliana kwa gharama za ndege na bili za hoteli.

 Na hii inaturudisha nyuma tulipoingia kwenye makala hii: Ni nani anayeongoza CBC kwenye suala la FBME? Mahakama ya usuluhishi iliziagiza pande zote mbili kufanya kazi kwa pamoja ili kuboresha usimamizi wa tawi, na kama tunavyowakumbusha mara kwa mara katika tovuti hii, wamiliki wa FBME, wakurugenzi na menejimenti mara nyingi wameonyesha nia yao ya kufanya hili litokee. Hadi sasa hakuna kitu, kilichotokea kwa upande wa CBC. Inawezekana kuwa sababu ni kwamba hakuna mtu mwenye mamlaka ambaye anaweza kuongoza? Hiyo itakuwa inaonyesha hali ya mambo ilivyo mbaya kwa CBC na kwa sekta ya benki nchini Cyprus kwa ujumla