Tunaomba msamaha kwa kutoonekana kwa Tovuti

Septemba 6, 2014

Waandishi wa tovuti hii kutoka FBME Limited wanachukua nafasi hii kuomba msamaha kwa kukosekana kwa tovuti wakati wa mchana na jioni ya tarehe 5 Septemba na tarehe 6. Tunaambiwa kwamba hii ni kutokana na kuwa tovuti hii kuwa ni sehemu ya  mashambulizi kutoka kwa ‘nchi nyingine ya Ulaya’. Inaonekana kwamba tumegusa mshipa wa fahamu mahali fulani; ukweli mara nyingi hufanya hivyo.

Mitandao ya Kijamii ipo hai na habari za uvumi. Ni nani au nini kimesababisha uzuiaji wa huduma hii yaweza kuwa ni swala la kuchunguzwa na matokeo yake yakawa ni kesi ya jinai chini ya sheria ya Ulaya. Kwa lolote lililotokea, tunasikia faraja kurudi mtandaoni kuweza kutoa maoni juu ya masuala muhimu  ya tabia isiyo ya kawaida ya viongozi waandamizi wa Cyprus.

Ni fursa nzuri, pia, kuwashukuru wale wote waliopo hapa na nje ya nchi ambao wamefanya kazi ngumu ya kutetea haki yetu ya uhuru wa kujieleza.