Ni Muda wa Uhakiki Thabiti wa Benki Kuu’

Februari 4, 2015

Akijibu shutuma kutoka kwa mmoja wa mjumbe wa bodi yake, Benki Kuu ya Cyprus imetangaza nia yake ya kufanya utafiti mkubwa kwenye shughuli zake kwa lengo la kuleta “marekebisho na utendaji wa kisasa”.

Mjumbe wa bodi ya CBC, Stavros Zenios, alionyesha kutoridhishwa kwake na wasimamizi waandamizi wa Benki Kuu ambao wanaonekana kutopenda mabadiliko muhimu yanayohitajika kufanyika. Aliandika katika blogu yake Februari 1 mwaka 2015, ‘Hii ni pamoja na usimamiaji mbaya wa migogoro ya kibenki katika historia ya nchi ambayo imeifadhaisha Cyprus. Anaongelea pia, ripoti ya waangalizi wa kimataifa ambao ilionyesha udhaifu ndani ya Benki Kuu. Ni wazi wanahisa wa Benki ya FBME, mameneja na wafanyakazi wake wana uzoefu wa jambo hili tangu pale walipoanzishiwa Azimio la Amri ya kulichukua tawi la Benki la Cyprus mwezi Julai 2014. Blogu ya Mheshimiwa Zenios ya Februari 1 ilisema ‘wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa Benki Kuu wanatambua haja ya mageuzi’. Amesifia ubora wa wafanyakazi, lakini akawalalamikia wasimamizi waandamizi ambao wanaonekana kuamini kuwa kila kitu kipo sawa. ” Hakuna cha Kubadilika ndani ya CBC, isipokuwa magavana,” aliandika.

Alitoa wito kwa utekelezaji wa mapendekezo kutoka kwa Kamati ya Lascelles kwenye ripoti yake juu ya mustakabali wa sekta ya benki nchini Cyprus, ambayo ilichapishwa Oktoba 2013. Aidha, aliandika, “… Benki Kuu ya Cyprus inaepuka matendo yoyote yanayoonyesha makosa na udhaifu wake, ” na kutaka uwazi mkubwa katika taasisi hiyo.

Kwa kuanzia, Gavana wa Benki Kuu alitangaza siku mbili baadaye (3 Februari) kwamba matokeo ya utafiti yataanza kufanyiwa kazi  ndani ya taasisi hii. Alisema baadhi ya tafiti zimeshaingizwa kwenye utekelezaji  na uamuzi ulichukuliwa Septemba 2014 “kuibadili na kuifanya CBC kuwa ya kisasa kabisa”. Hii ni sehemu ya kuzidi kuitambua Benki Kuu kwamba ni taasisi inayoisababishia nchi kuwa kwenye hatari.

Pendekezo:
Tovuti hii ingependa kutoa mchango mmoja kwenye masuala mbalimbali kwenye utafiti wa Benki Kuu ya Cyprus kwamba miongoni mwa hatari zinazoikabili Benki Kuu ni suala la kushindwa kwenye mamlaka ya usimamizi.

Kushindwa kwa taasisi kadhaa za benki nchini Cyprus katika miaka michache iliyopita linaweka rekodi kwa umma. Ni wazi, Benki Kuu haikuweza kuzuia haya yasitokee kama ilivyopaswa kufanywa. Katika shughuli zake za usimamizi Benki Kuu inapaswa kutazama mambo kwa jicho la ukaribu sana (au macho nne, kama inavyopendekeza kwa mabenki kufanya) ili kupunguza mabaya yanayoweza kutokea. Lakini kuna tabia ya mamlaka ya usimamizi kulala usingizi wakiwa kazini. Matokeo ambayo yanaleta swali kama wasimamizi waandamizi wa benki kuu wana utaalamu unaofaa au la. Vile vile, matumizi mabaya ya Azimio la Amri kwa Benki ya FBME tawi la Cyprus limeiingiza nchi kwenye hasara kutokana na madai ya fidia. Kutafuta ufumbuzi inaweza kuisaidia Jamhuri kuondokana na matatizo yanayoiweka nchi njia panda.

Kama wafanyakazi wa Benki  Kuu wanatakiwa kutumika kama wasimamizi wa fedha kuna haja ya kuundwa aina fulani ya ukaguzi wa ujuzi wao na ufanisi – sawa na ‘Kipimo cha Ufanisi’ kinachotumika kwa wasimamizi waandamizi wenye miaka mingi. Vipimo hivi vimeundwa ili kuzuia watu wasiofaa kuendesha benki na itekelezwa na Benki Kuu ya Cyprus kama sehemu ya mchakato wake wa wasimamizi. Kushindwa kwa wasimamizi muhimu ndani ya benki Kuu kupita vigezo hivi kutawazuia kuteuliwa kwenye nafasi zinazopendekezwa kwao au hata Taasisi husika kunyimwa leseni. Wakati Vipimo vya Uthabiti’ haviwezi kuondoa kabisa hatari ya kushindwa kimfumo, vinaweka viwango dhidi ya utendaji kazi ambapo mafanikio na ubora wa kazi unaweza kupimwa.

Kuna ulazima wa moja kwa moja kuvikubali vipimo hivi kwa wale wanaoshikilia nafasi za juu ndani ya Benki Kuu. Wale walio na majukumu ya usimamizi ni lazima wawe na sifa, ujuzi na uzoefu wa kutekeleza majukumu walioteuliwa kuyafanya. Kwa mfano, kama mtu anayekagua benki anapaswa kuwa na ufahamu wa kibenki, vivyo hivyo watu walioajiriwa kutekeleza usimamizi ulio bora wa mabenki lazima awe na uzoefu katika benki. Uborakiwe ndio kigezo cha kumteua mtu na sio uteuzi wa kisiasa.Usimamizi wa benki na huduma nyingine za fedha hauwezi kuachwa kuwa holela. Siyo kitu ambacho unaweza kujifunza ndani ya dakika tano na haifai kabisa kujaza nafasi za juu kwa uteuzi wa wanasiasa hata kama wamefanya vizuri kwenye maeneo mengine.

Kama wafanyakazi wa mabenki ya biashara wanapewa ‘Vipimo Thabiti ‘, vivyo hivyo na Benki Kuu pia. Hakuna kukubali vinginevyo

P.S. Kwa bahati njema, kila Mkurugenzi wa Benki ya FBME Limited na kila Mkurugenzi wa Kitengo cha Kadi cha FBME Limited, na wasimamizi waandamizi wa vyombo nyote viwili, wamepitia na kufaulu vipimo Thabiti. Pamoja na msaada wa takriban wafanyakazi  wengine 400 – na mamia zaidi waliokuwepo kabla yao – wamejenga, kwa zaidi ya miaka 30, ‘Benki yenye Viwango Bora’.