Dhambi: Zile za Mapungufu na Zile za Utendaji

9 Mei 2015

Tarehe 21 Julai, 2014 mnamo saa 5 usiku, Benki Kuu ya Cyprus ilitangaza kuanza kwa hatua ya Azimio kwa tawi la benki ya FBME la Cyprus. Kama tujuavyo, Azimio ni njia inayotumika kwa uendeshaji wa shughuli zote za benki inayofilisika, lakini haijatumika kwa benki iliyo na fedha, yenye ukwasi wa kutosha kama FBME tawi la Cyprus. Katika kuifikia hatua hii, Benki Kuu ilishindwa kuratibu – au hata kuijulisha – Benki Kuu ya Tanzania ambayo ni Msimamizi Mkuu wa Makao Makuu ya Benki ya FBME. Kuanzia siku hiyo hadi sasa, CBC imeshindwa kuunganisha matendo yake na yale ya mamlaka kuu nchini Tanzania au hata kufuata kanuni na sheria za Cyprus na Umoja wa Ulaya (EU).

Moja ya sababu za uogo zilizopatikana kwenye vyanzo visivyo rasmi kwa maofisa wa CBC ni kwamba Kamati ya Azimio, inayomjumuisha Gavana na Wakurugenzi wake Watendaji wawili, hawakuwa na uamuzi mbadala. Hili si kweli. Walikuwa na mbinu mbadala iliyopendekezwa na wakurugenzi na uongozi wa Benki ya FBME ambayo kamwe hawakuijibu, na kulikuwa na baadhi ya fursa nyingine pia.

Uongo mwingine ni kwamba Benki mwambata zilikataa kufanya miamala na Benki ya FBME, ambao tena haukuwa na ukweli.

Tetesi ya tatu ilikuwa kwamba uamuzi wa kuchukua hatua hizi kwa tawi la FBME la Cyprus ulitolewa na Mamlaka ya Azimio. Tunajua kutokana na kujiuzulu kwa Stavros Zenios kutoka Bodi ya CBC mwezi Machi, kuwa hii haikuwa hivyo. Alikuwa mjumbe wa Mamlaka ya Azimio kwa wakati huo na amesema hadharani kwamba hakushauriwa. Baada ya hapo alipendekeza uchunguzi ufanywe kwa kile kamati ilichokuwa ikikifanya, pendekezo ambalo lilikataliwa na wajumbe watatu wa Kamati.

Hii ilisababisha mfululizo wa ‘mapungufu’, ambapo kanuni za msingi za Mwongozo wa Basel juu ya Usimamizi wa Mabenki na kanuni za Ulaya za Kuinusuru benki na Maelekezo ya Azimio vilipuuzwa.

Maelekezo ya EU kuhusu matumizi ya Azimio juu ya benki yanasema: Lengo lazima liwe “… (1) Kulinda mwendelezo wa shughuli muhimu za kibenki, (2) kulinda wateja, mali za mteja na fedha za umma, 3) kupunguza hatari kwa utulivu wa kifedha, na 4) kuepuka uharibifu usio wa lazima wa thamani. “CBC haikuonyesha kujali hata kidogo kuhusu maelekezo hayo.

Miongozo ya Basel inasema Azimio liundwe tu kwa ajili ya benki ambazo ni nyonge – (Muhtasari), “Katika hali ya kawaida,” Mwongozo unasema, “ni wajibu wa bodi ya wakurugenzi na mameneja waandamizi wa benki, na si msimamizi, kuamua jinsi benki itakavyotatua matatizo yake “(Mwongozo wa 106).

“Msimamizi wa Nyumbani (katika kesi hii BoT) na Msimamizi wa nje (CBC) ni lazima “kushirikiana kwa taarifa na mambo yote kwa ajili ya usimamizi na ufanisi wa vyombo vyake ikiwa ni pamoja na kuratibu mwitikio wa usimamizi kwa ajili ya utunzaji bora wa mazingira ya mgogoro, “(mwongozo 251).

Mwongozo wa 94 unasema, “msimamizi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Azimio (kama ipo) anatakiwa kuandaa mpango yakinifu na wa kina utakaoshuhulika na benki dhaifu ili kukabili vema mgogoro uliopo.” Hakuna mtu aliyeuona mpango kama huo kutoka CBC au wasimamizi wake, uwe wa kina au vinginevyo.

“Benki na msimamizi wanapaswa kuchukua hatua za haraka ili kuzuia matatizo ya kukua na kuchochea udhaifu wa fedha wa benki,” (Mwongozo wa 108). Vitendo vya CBC vilikuwa ni kinyume chake kabisa.

Upungufu mwingine ni kushindwa kwa CBC kushirikiana na wachunguzi walioteuliwa na Bunge la Cyprus. Orodha inaendelea.

!!!!!

Sasa Tuangalie dhambi ya Utendaji: Mambo ambayo CBC na msimamizi wake Dinos Christofides wameyafanya.

Hawakupaswa kamwe kutumia sheria ya benki inayofilisika, hasa ile iliyoundwa kwa ajili Benki ya Laiki, na kujaribu kuilazimisha kwenye benki yenye afya.

Hawakupaswa kulifunga tawi la FBME la Cyprus kwa kuzuia miamala na shughuli zote kuanzia tarehe 24 Julai hadi Septemba 2, 2014 wakati Sheria ya Cyprus inasema wanaweza kufanya hivyo kwa siku nne tu za kazi.

Christofides hakupaswa kujiwakilisha mwenyewe kwa maandishi na kwa njia nyingine ya kuwa ana jukumu juu ya benki nzima (ili kudai na kuzipata amana za FBME), wakati yeye aliteuliwa kama msimamizi wa tawi la Cyprus.

Wakati alipolifungua tawi ili kuendelea na miamala Septemba 2, 2014 kwa msaada wa CBC, Christofides alipaswa kutoa maelezo ni kwa nini alipunguza viwango kwa wateja hadi EUR 10,000 kwa siku, kisha kupunguzwa hadi EUR 5,000 kwa siku na hadi kiwango cha sasa cha EUR 200 .

Christofides alisitisha uendeshaji wa akaunti kama 300 tokea Septemba, na kuzifungulia tena mwezi Novemba bila maelezo yoyote.

CBC iliruhusu mara kadhaa uchunguzi kwa tawi la FBME Cyprus katika kipindi cha 2014. Baadhi ya uchunguzi ulifanywa na kampuni ya kimataifa PwC na mwingine na wafanyakazi wa CBC yenyewe. Hakuna matokeo yoyote yaliyochapishwa. Kama wangechapisha, wangeweza kusaidia kujibu madai ya awali ya FinCEN. Msimamizi wa CBC pia alizuia kazi ya wachunguzi wa kihasibu na wanasheria wa kimataifa wa Marekani walioteuliwa na wamiliki wa FBME kuichunguza benki

Sasa, CBC amemteua msimamizi wa pili. Uchunguzi mwingine umeanzishwa kwa mbwembwe na vitisho, ukijumuisha Kroll, DLA Piper na Georgiades & Pelides. Baada ya kutoambulia chochote katika kipindi cha miezi tisa, kinachoonekana sasa ni marudio ya mchezo wa CBC, kwa sasa ikiwa na gharama kubwa zaidi. Ingawa FBME Limited ina maswali mengi kwa mbinu iliyopitishwa ya kufanya uchunguzi mwingine, bado itatoa ushirikiano kamili.

Mbali na kutishia wafanyakazi wa FBME na kusababisha hasara ya ajira katika makampuni mbalimbali na wateja – ndio hivyo. Baada ya kazi ya miezi tisa, wakati ambao madhara mengi yamepatikana, haya ndio wanayotuonyesha.

 

 

 

.