Wanahisa Wadai Dola Milioni 500 kama Gharama ya Uharibifu

Novemba 28, 2014

 

Hati ya Usuluhishi katika kesi iliyofunguliwa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Biashara (ICC) na wamiliki wa FBME Limited, kampuni tanzu  ya Benki ya FBME, inaonyesha kwamba madai ya madhara dhidi ya Jamhuri ya Cyprus yanakadiriwa kufikia Dola za Kimarekani nusu bilioni kwa sasa.. “lakini kuna uwezekano wa kuzidi kiasi hiki wakati kesi ya  usuluhishi itakapokamilika.” ICC ina mamlaka ya mwisho ya kuamua  juu ya madai ya gharama za uharibifu huu. Nakala ya muhtasari wa hati ya usuluhishi inapatikana hapa

FBME Limited inatumia kipengere cha mkataba wa makubaliano ya kimataifa kati ya Cyprus na Lebanon uliosainiwa tarehe 19 Machi 2003, unaolinda haki za mwekezaji katika kila nchi. Mkataba huu ulipuuzwa na Benki Kuu ya Cyprus wakati ilipotangaza Azimio la Amri dhidi ya tawi la FBME Cyprus tarehe 21 Julai 2014, ambayo ilichukua uongozi wa tawi kimabavu na kufanya jaribio la kuliuza tawi la Benki bila idhini ya wamiliki. Tangu wakati huo, wamiliki wa Benki wameingia kwenye  mapambano ya kisheria dhidi ya matendo ya Benki Kuu ya Cyprus na Msimamizi wake aliyetumwa kuendesha tawi kidikteta.

Hati ya  usuluhishi inaonyesha kiundani madhara yaliyosababishwa na vitendo vya Benki Kuu vya haraka, vilivyokuwa na nia ya madhara. Hati hiyo pia imeweka wazi  madhara yanayoendelea kusababishwa kwa Benki na wateja kwa vitendo vya Msimamizi, Mr Dinos Christofides. Hii imejumuisha kufungwa kwa tawi kutoka Julai 22 hadi Septemba 2, kuzuia miamala tangu mapema Septemba, na jaribio lake … “la kufyonza ukwasi wa tawi kwa faida ya CBC (Benki Kuu ya Cyprus)”. Yeye pia … “alikataa kuchukua hatua yoyote muhimu kuruhusu Benki ya FBME kufanya miamala fulani kwa sarafu isiyo USD” na pia … “alizuia kabisa juhudi za Benki kufanya hivyo kwa uwezo wake yenyewe”. Hati pia inaonyesha jinsi akaunti za tawi la FBME Cyprus zilipofungiwa na Msimamizi bila kuwa na sababu ya msingi.

Kama wamiliki na mameneja tunaowajibika, wanahisa wanaitia hatiani Jamhuri ya Cyprus kwenye mahakama ya usuluhishi kwanza ili kulinda Benki, wafanyakazi na wateja, lakini pia walipa kodi wa Cyprus … “ambao hatimaye watalipa gharama za uharibifu zitakazolipwa kwa wanahisa kufuatia kukosekana kwa uwajibikaji na vitendo haramu vya CBC “.

ICC ilikubali kufungua jalada kwa ajili ya usuluhishi na wanahisa wa Benki ya FBME tarehe 28 Oktoba. ICC iko Paris na ni chombo cha kidunia kinachoongoza kwenye masuala ya usuluhishi wa migogoro ya biashara ya kimataifa.

Katika utangulizi wake kwenye kitabu cha kanuni cha usuluhishi, ICC anaandika: “Usuluhishi chini ya Kanuni za Usuluhishi za ICC ni taratibu zilizo rasmi ambazo zinapelekea maamuzi ya kisheria kufanyika kutoka mahakama isiyofungamana na upande wowote, inayohusika na utekelezaji kwa mujibu wa sheria za usuluhishi za ndani pamoja na mikataba ya kimataifa kama vile Mkataba wa New York wa mwaka 1958 “.