Kila Mmoja Anaathirika na Sakata hili

19 Julai 2015

Tarehe 17 Julai 2014, mlolongo wa matendo ulianzishwa ambao ulikuwa na madhara makubwa kwa wateja, wafanyakazi na washirika wa Benki ya FBME, ndani na nje ya nchi. Watu wamepoteza kazi zao na makampuni yamefungwa. Aidha, kuna waathirika wengine ambao wameanza kuhisi athari kwa sasa – walipa kodi, serikali, mamlaka ya benki na mfumo wa haki wa kisiwa cha Cyprus. Katika ujumbe huu, Benki ya FBME inatoa maoni yake juu ya nini kimetokea.

Kwa taarifa zaidi juu ya suala hili na kilichoandikwa hapa, tembelea www.fbmeltd.com

Inatisha ukifikiri kwamba mwaka umepita tangu uamuzi mbovu wa Kamati ya Azimio ya Benki Kuu ya Cyprus (CBC) kuliendesha tawi la Benki ya FBME katika kisiwa cha Cyprus.. Kuanzia siku hiyo hadi leo, vitendo vya Kamati ya Azimio vimebaki vile vile vilivyokuwepo mwaka mmoja uliopita: Visivyo tabirika, visivyo vya kitaaluma, vyenye kisasi na huenda kukiwa na uwezekano wa njama ndani yake.

(Angalia www.fbmeltd.com/termsexplained kwa maana ya Kamati ya Azimio na vyombo vingine.)

Lengo letu kwa kuandika ujumbe huu ni kuwajuza watu kuhusu maoni yetu juu ya nini kilichotokea na kuwatahadharisha na madhara ya vitendo vya baadhi ya maofisa. Kuna njia ya kukomesha sintofahamu hii nasi tunatumia waraka huu kuelekeza kwenye njia ya kutafuta ufumbuzi.

Hakuna washindi katika sakata hili na wadau wachache wanaweza kuepuka madhara makubwa. Benki ya FBME na matawi yake ya Cyprus imeatirika – na inaonekana kama imefanyika kwa makusudi! Maslahi ya wateja wa Benki yameharibiwa. Kuna waathirika wengine wasio na hatia kwa kutowajibika kiutalaamu kwa Kamati hii ya Azimio, ikiwa ni pamoja na Serikali na watu wa Jamhuri ambao wanakabiliwa na kuongezeka kwa madai ya fidia.

Sifa ya Cyprus kama kituo cha benki na uwekezaji imeharibika. Maswali makubwa yameulizwa juu ya mfumo wa kisheria na umahiri wa wasimamizi mfumo wa kifedha. Na hali ilendelea kuwa mbaya siku hadi siku. Hata hivyo inawezekana kusema imetosha. Ni nani yupo tayari kuchukua uamuzi huu na kuelekea mbele?

Huenda lawama kubwa inaweza kuwekwa mlangoni pa Kamati ya Azimio ya watu watatu (kwa sasa wawili baada ya mmoja kuachia ngazi) na Mamlaka ya Azimio yenye mtu mmoja kwa maamuzi yao yasiokuwa ya lazima na mara zote yameelekea kushindwa. Hata hivyo, maamuzi yao yamebeba adhabu kubwa kwa wote wanaohusika. Hii inaonyesha nini kinaweza kutokea wakati taasisi kama CBC inafanya maamuzi bila kuwajibika kwenye sekta ya fedha, serikali, viongozi wa kuchaguliwa au mahakama.

Usiku wa Julai 21, 2014, kwa sababu ambazo hazikuelezwa, Kamati ya Azimio ya CBC ilitumia sheria ya Azimio kuliendesha tawi la FBME la Cyprus.ilifanya hili kwa kumteua mtu wao wenyewe kuwa Msimamizi, lakini aligeuka kuwa mbovu na mwenye migongano ya kimaslahi. Tangu mwanzo, msimamizi wa CBC aliongoza kinyume na maslahi ya wateja wa Benki kwa kuanza kuzuia upatikanaji wa fedha. Mara baada ya kuruhusu upatikanaji wa Fedha aliweka vikwazo visivyofaa na kusababisha mkanganyiko zaidi kwa wateja.

Mishahara haikuweza kulipwa, bili za haraka hazikuweza kulipwa kwa wakati, watu wamepoteza ajira zao na makampuni yamesimamisha utendaji. Yote haya yamefanyika kwenye uchumi wa Cyprus inayokabiliwa na mtikisiko wa kiuchumi!

Kwa upande wao, wajumbe wa Kamati ya Azimio walidhoofisha mahusiano na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), makao makuu ya msimamizi wa FBME katika kesi hii. Uamuzi wa kuweka sheria ya Azimio kwa tawi la FBME Cyprus ulikuja kwa mshangao kwa BoT kama ilivyokuwa kwa Benki. Kwa mshangao, CBC ilikataa ushirikiano kama inavyotakiwa na taratibu za kimataifa na kuchukua maamuzi ambayo yaliharibu maslahi yao wenyewe na ya watu wengine. Hadi leo hii, Kamati ya Azimio halijaliweka sawa suala hili.

 

Madai ya FinCEN

vitendo vya Kamati ya Azimio vilifuatia madai ya ofisi ya hazina ya Marekani FinCEN kwamba FBME ilikuwa na mifumo mibaya ya kupambana na fedha chafu. Uchunguzi uliofanywa na vyombo vya kimataifa kama vile Ernst and Young ya Marekani, Hogan Lovells ya Marekani na KPMG ya Ujerumani hawakugundua ushahidi wowote wa madai hayo. FBME inaendelea kushirikiana na FinCEN kumaliza kabisa madai hayo. CBC, kwa njia yoyote, haijajibu madai hayo.

Jinsi gani Kamati ya Azimio ialivyochukua uendeshaji wa tawi la FBME ilikuwa ni kwa kutumia sheria isiyofaa ya Azimio, ambayo ilipitishwa chini ya shinikizo kubwa mwaka 2013 ili kukabiliana na Benki ya Laiki, ambayo ilikuwa imefilisika na haina ukwasi. Hii kamwe haikutakiwa kutumika kwa FBME ambayo ilikuwa na afya na ukwasi wa kutosha (angalia, hadithi ya Benki ya FBME nchini Cyprus).

Sheria ya Azimio inahitaji masharti matatu kuwepo kwa benki inayofilisika, hakuna hata sharti moja linaloweza kutumika katika kesi ya FBME.

Ni muhimu kukumbuka kwamba kile FinCEN walichokisema ilikuwa ni tuhuma tu na Benki ilipewa siku 60 kutoa majibu yao. Hakukuwa na sababu kwa Kamati ya Azimio kuchukua hatua, na badala yake, ilitarajiwa kwamba CBC ingeisaidia FBME kusafisha jina lake ukizingatia kwamba hata Cyprus na mamlaka yake ya usimamizi nayo pia ilihusishwa na tuhuma za FinCEN na kudaiwa kwamba CBC ilikuwa na jukumu la kusimamia tawi la FBME Cyprus kwa zaidi ya miaka 30.

Viongozi waandamizi wa CBC walihusishwa na tuhuma kwa njia mbalimbali.. MOKAS, idara ya kuchunguza maovu ya kifedha nchini Cyprus ilikiri kwamba ilipokea waraka wa FINcen na kuupeleka CBC. Kwa nini CBC haikuwatahadharisha FBME au kuchukua hatua za kukanusha tuhuma hizo ilizotambua kuwa si za kweli imebakia kuwa siri kubwa. Moja ya madai hayo ni yalikuwa FBME ilikuwa inakabiliwa na faini ya takriban Euro milioni 240 mnamo mwaka 2013 ambazo zilikuwa hazina hata chembe ya ukweli. Maombi kwa CBC, pengine yenyewe ni chanzo cha uvumi, kuchunguza jambo hili yamekutwa na ukimya mkuu. Aidha, Msimamizi maalum wa CBC amekuwa akijaribu kuizuia Benki kuthibitisha kutokuwa na hatia kwa kuwazuia wachunguzi wa kimataifa Ernst and Young kuingia kwenye tawi la Benki la Cyprus.

Je, hii ni njia ambayo CBC, Kamati yake ya Azimio na mawakala wake wanapaswa kufanya kulinda utulivu wa kifedha katika sekta ya benki nchini Cyprus?

 

Uchunguzi wa CBC yenyewe

CBC anaijua ukweli kuhusu utendaji wa FBME kwani ni msimamizi muda mrefu wa tawi la Benki hiyo. Mara kabla na tangu tangazo la FinCEN, CBC imekamilisha uchunguzi wake yenyewe uliofanywa na wataalamu wa kimataifa kutoka PWC na Kroll, na wafanyakazi wa Benki Kuu. Kutokana na umuhimu wa ufahamu wa chunguzi hizi, ni ajabu kwamba hakuna matokeo yaliyowekwa wazi kwa FBME kama yeyote alivyotarajia!

 

Kuna swali jingine kuhusu matumizi ya Kamati ya Azimio kutumia fedha za wateja wa FBME, bila kibali kutoka Benki au wateja wenyewe, au matumizi ya zabuni yasiyo sahihi.

Wasimamizi Maalum wawili wameteuliwa na wengine kama vile wanasheria, wafilisi, makampuni ya usalama na wapelelezi wamekuwa kwakilipwa kutoka kwenye amana za FBME. Msimamizi wa kwanza, Dinos Christofides, aliteuliwa mwezi Julai 2014 na alijiuzulu ghafla miezi 10 baadaye, na vitendo vyake vinapaswa kuchunguzwa kisheria. Msimamizi wa pili analipwa mara tano zaidi ya wa kwanza, ingawa yeye ni nadra sana kuwepo nchini Cyprus.

Kama tulivyoeleza, hatua hizi zote hazikuwa na ulazima kabisa, ambazo zinasababisha mtu kudhani kama kuna mkono wa siri nyuma haya yote: kila kitu kinatokea kwa sababu Fulani na kama hakuna sababu, basi kuna sababu ya kuwa hayo pia! Kama CBC ingefanya kazi na waandamizi wa Benki, kama ilivyotarajiwa, juhudi kubwa zingefanywa ili kuhakikisha madhara kwa waathirika yangepunguzwa sana.

FBME imeomba kwa mara kadhaa kupata ufafanuzi kutoka CBC na mawakala wake bila kupata majibu, wakati juhudi kama hizo kutoka kwa mdhibiti mkuu BoT, nazo zimekuwa zikipuuzwa. CBC walidhani wangeweza kuwashinikiza wenzao wa nchini Tanzania lakini wamejifunza kwa gharama kuwa hawawezi. Pia ilipuuza utatuzi wa kimataifa wa sekta ya fedha, ambayo ilifanya juhudi kuizuia CBC kutochukua udhibiti wa Fedha za wateja wa FBME kama CBC ilivyojaribu kufanya mara kadhaa.

 

Vitendo Vinahitajika Sasa

Hivi sasa, inaonekana kwamba viongozi waandamizi wa CBC wamepooza kwa kuandamwa na mfululizo wa kashfa, moja tu kati ya hizo inahusu FBME. Kusaidia kuzuia kupooza huku kubaya, FBME inatangaza hadharani sasa nia yake ya kushirikiana na viongozi wa CBC kutafuta njia kusitisha kadhia hii. Hapa ni orodha ya awali kuhusu masuala ambayo tunapaswa kufanyia kazi:

  • Kuwe na makubaliano kati ya wasimamizi waandamizi wa FBME na CBC juu ya mpango mkakati kwa ajili ya kuianzisha tena Benki na kitengo cha huduma za Kadi cha FBME. Hii lazima iwe kipaumbele kikuu.
  • Kuwe na ushirikiano kamili katika kuendeleza uhusiano na Mabenki mwambata wa FBME (Correspondent Banks).
  • matokeo ya uchunguzi wote uliofanywa kwa niaba ya CBC, unapaswa kutolewa pamoja na taarifa ya Kamati ya Azimio.
  • CBC na wasimamizi watendaji wa FBME washirikiane kwa uaminifu na ukamilifu kwa ajili ya kuanza huduma za Reuters, Bloomberg na Euroclear.
  • Mawasiliano ya msingi na ya kuheshimiana yanapaswa kuanzishwa kwa BoT na mawakala wake, wamiliki wa FBME na wasimamizi.
  • FBME ina hamu kubwa ya kuufanya upya ushirikiano wake na mamlaka za Cyprus ili kurejesha imani katika sekta ya benki ya Jamhuri na kurudi kwenye nafasi yake katika kujenga uchumi wa nchi.

Hakuna hata moja kati ya mambo haya kuwa ni tatizo na yote yanatekelezeka kiurahisi. Ni mwanzo tu lakini ni hatua muhimu ya kwanza. Sisi Tunasubiri kusikia kutoka Benki Kuu.

 

Hadithi ya Benki ya FBME Nchini Cyprus

Benki ya FBME ilianzishwa nchini Cyprus mwaka 1982 kama kampuni tanzu ya Federal Bank of Lebanon (FBL), yenyewe ikiwa imeanzishwa mwaka 1952. FBME ilimilikiwa kwa 51% na Michel Saab, na zilizobaki 49% zilimilikiwa kwa usawa na Ayoub-Farid M Saab na Fadi M Saab. Baada ya kufariki kwa Michel Saab mwaka 1991, hisa zake zilikwenda kwa Ayoub-Farid Saab na Fadi Saab kwa viwango sawa. Kuhamia kwa FBME kutoka Cyprus kwenda visiwa vya Cayman na hatimaye Tanzania ilikuwa ni kutokana na sera za CBC kutokukubali jukumu la kuwa mdhibiti mkuu.

Katika kipindi cha miongo mitatu Benki imechangia kwa kiasi kikubwa nchini. Kwa mfano, katika miaka sita na nusu kabla ya hatua za Azimio Julai 2014 FBME ilikuwa mmoja kati ya walipa kodi wakubwa wa sekta binafsi katika kisiwa cha Cyprus. Ifuatayo ni muhtasari wa mchango na Benki kwa kipindi kuanzia mwanzo wa 2008 hadi katikati ya 2014:

  • Matumizi ya mali, ikiwa ni pamoja na majengo mapya, vifaa vya ofisi, magari nk: EUR milioni 15.6
  • Gharama kwa bidhaa za ndani na huduma katika Cyprus EUR Milioni 28.5

 

  • Jumla ya gharama za wafanyakazi ikiwa ni pamoja na mishahara EUR milioni 51.6

 

  • Kodi kwa Cyprus na malipo ya bima ya kijamii EUR milioni 38.3

 

Jumla EUR 134.0 milioni

 

Misaada mingine kwa Cyprus imepatikana kupitia mikopo na uwekezaji. Mwaka 2012, FBME imewekeza EUR 240 milioni nchini Cyprus kama deni huru wakati Nchi alipokuwa inaingia kipindi kigumu cha mgogoro wa kifedha, Kaika nusu ya kwanza ya mwaka 2014 Wizara ya Fedha iliandika katika matukio mawili tofauti kuishukuru Benki kwa msaada wake, na kabla ya tangazo la Amri ya Azimio kulikuwa na makubaliano ya uwekezaji zaidi wa takriban dola milioni 300.

FBME pia imewekeza EUR milioni 30 nchini Cyprus kwenye Mamlaka ya Umeme wakati wa maafa ya Mari mwezi Julai 2011, wakati mgumu kabisa kwenye mlipuko wa Amani nchini. Benki pia ilionyesha nia yake ya baadaye kwa Cyprus kwenye ujenzi wa jengo jipya Nicosia.

Kabla ya hatua ya Kamati ya Azimio, afya ya kifedha ya FBME tawi la Cyprus na ya Benki ya FBME kwa ujumla, ilikuwa na ubora wa kipekee. Mwezi Julai 2014, hesabu mizania, kama ilivyotayarishwa na wakaguzi wa nje wa FBME, ilikuwa:

Uwekezaji dhidi ya amana 84.15%

Uwekezaji na Hati fungani dhidi ya amana zote 104.44%

Mikopo Yote dhidi ya Amana 15.95%

Mikopo dhidi ya Amana 10.95%

 

Ukiritimba wa Malipo

Uamuzi wa wakala Kamati ya Azimio, msimamizi maalum wa kwanza, alipozuia wateja kutochukua Fedha alisababisha Kitengo cha Huduma zaKadi cha FBME kupunguza wafanyakazi 70 (tazama www.fbmeltd.com//media-identify-link-with-monopolistic-card-market/). Wakati huohuo iliharibu ushindani katika biashara ya kadi, kupandisha bei ya huduma hiyo na kudhoofisha faida. Inasemekana kwamba soko la shughuli za Kadi la Cyprus kwa mara nyingine ndio pekee lenye ukiritimba katika soko la Ulaya.

Mamlaka ya Azimio Cyprus

Mamlaka ya Azimio ni chombo kinachowajibika na kuweka hatua za Azimio juu ya benki nchini Cyprus lakini inaonekana kwamba Mamlaka, zikiwemo na Bodi ya Wakurugenzi CBC haikuchukua maamuzi juu ya Benki ya FBME tawi la Cyprus. Kwa kukiuka sheria maamuzi haya yalichukuliwa na Kamati ya Azimio, ambayo Gavana na Wakurugenzi wawili Watendaji wa Bodi walitekeleza. Mmoja wa wakurugenzi hawa watendaji amejiuzulu.