Nini hasa kilichotokea kwenye Kitengo cha Huduma za kadi cha FBME

Septemba 9, 2014

Ukweli wa msingi uliosababisha kusimamishwa kwa shughuli kwenye kitengo cha Kadi unajulikana vizuri: Kabla ya saa 5 usiku wa tarehe 21 Julai 2014, Benki Kuu ya Cyprus ikitolea mfano tangazo la FinCEN la Julai 17, walitekeleza Azimio la amri dhidi ya tawi la FBME Cyprus. Hii ilisababisha kupiga marufuku maramoja shughuli zote za FBME Cyprus ambayo ilidumu hadi tarehe 2 Septemba, hatua ambayo iliinyonga Idara ya huduma za Kadi ya FBME

Hakukuwa na njia nyingine kwa idara hii iliyokuwa na leseni ya kujitegemea kama kampuni. Tarehe 7 Agosti shughuli zote zilisitishwa na madai yote ya wateja wa wa kadi walilipwa.  Tarehe 11 Agosti, wafanyakazi 72 wa kitengo hicho walipunguzwa kazini huku watatu zaidi wakiwekwa katika tahadhari na kubaki na wafanyakazi 30 tu. Wafanyakazi wengi walioachishwa walikuwa na uzoefu wa miaka mingi na thamani kubwa; athari za kupunguzwa kwao kazi itawakumba wao na familia zao; lakini pia nchi itapata  athari kubwa kutokana na uachishwaji wa kazi huu.

Awali ya yote, kuna gharama kubwa ya uachishwaji kazi katika nchi inayokabiliwa na kuongezeka uchumi dhaifu ambapo maelfu tayari wameshafukuzwa kazi. Halafu kuna hasara ya mapato ya kodi ya baadaye kutoka kwenye  Kampuni na kutoka kwa wafanyakazi wake. Kuna athari pia kwa wafanya biashara na mengine mengi. Kwa kila mtu aliepunguzwa, wengi zaidi moja kwa moja watakuwa wameathirika.

Halafu kuna athari juu ya huduma za kadi kwa ujumla. Labda kama kungekuwa na makampuni kadhaa ya kadi hali hii ingeweza kupungua. Lakini nchini  Cyprus kulikuwa na makampuni mawili tu yaliokuwa yakifanya kile kinachoitwa ‘acquiring’. Ikiwa na maana ya kuweka mashine na vifaa vingine kwenye mahoteli na maduka mbalimbali na migahawa  ili kuwezesha ufanyaji wa biashara na malipo kati ya wateja ‘Merchants’ na mabenki . Kwenye huduma hii makampuni hutoza gharama kwa asilimia fulani kwa kila muamala.

Kabla ya Agosti mwaka 2014, makampuni mawili nchini Cyprus yaliyokuwa yakifanya biashara hii kama ‘acquirer’ yalikuwa ‘JCC Payment Systems’ na ‘IMSP’ ambacho ni kitengo cha Kadi cha FBME – sasa kuna kampuni moja tu. Kwa FBME kuwa nje ya uwanja kuna athari kubwa kwa JCC.

Kwanza, Historia Yake: JCC ilianzishwa mwaka 1989 na awali ilimilikiwa na taasisi 10 za fedha. Leo hii, Benki of Cyprus ina asilimia 75% ya hisa za biashara na wengine ni  muungano unaohusisha Benki ya  Hellenic, Benki ya Taifa ya Ugiriki, Benki ya Piraeus na Benki ya Alpha. Mwanzoni, JCC ilikuwa inahodhi soko lote na kiwango cha ada yake kwa wafanyabiashara kilionyesha hali hii ya ukiritimba. Viwangi vilikuwa juu sana pengine kuliko vyovyote katika EU – hiyo ndiyo tabia ya ukiritimba. Hakika hii ilichangia kwa bei za jumla za malipo kwa ajili ya bidhaa na huduma nchini Cyprus, kuwa ghali kwa kipindi kirefu sana.

Kilichobadilisha hali hii ilikuwa ni IMSP, ambayo ilianza kutoa huduma ya ‘acquirering’ kimashindano kwa wafanyabiashara katika mwaka 2008. Huduma hii iliyoanzishwa na kundi la wafanyabiashara vijana wa Cyprus, IMSP ikaanza kupata mafanikio ya haraka. Ilitoa  teknolojia bora zaidi kama vile mashine za kadi  katika vituo vya biashara; kupunguza ada ya muamala kwa wafanyabiashara kwa nusu ya kiwango JCC, na pia ilianzisha huduma ya malipo ya siku-ijayo na kufanya mfanya biashara kupata malipo ya huduma ndani ya masaa 24 ukilinganisha na ya siku tatu iliyotolewa na JCC.

JCC ilijibu kwa kufyeka viwango vyake yenyewe na kuzidisha ubora wa huduma zake. Kutokana na  ukweli kwamba ada hulipwa na mlaji wa mwisho, ni wazi kwamba uanzishwaji wa IMSP kuliweza kuokoa mamilioni ya Euro kwa wamiliki kadi wa Cyprus. Ushindani ulionyesha nini ushindani daima unafanya; : faida pande zote katika mazingira bora.

Uwezo wa IMSP ulikuwa wazi. Benki ya FBME ikainunua kampuni hii na wafanyakazi wake mwaka 2012 katika makubaliano ya kirafiki. Tangu wakati huo IMSP imekuwa sehemu ya Kitengo cha Huduma Kadi cha FBME

JCC ilijibu kwa kukabiliana na ushindani hatua iliyowalenga  wateja wa FBME. Kwa miaka mitano iliyopita kumekuwa na uchunguzi uliofanywa na mamlaka husika kuhakikisha kwamba ushindani kwa wote ni wa haki sawa katika nchi – Hii ni tume ya Ushindani ya Cyprus.
Uamuzi wa awali ulipatikana katika Kitengo cha Kadi cha FBME mwezi Aprili 2014 na FBME itaendelea kusaidia uchunguzi huu hadi hitimisho lake: ni muhimu kwa Jamhuri ya Cyprus kuhakikisha kwamba hili linafanyika. Kwamba masoko yote yanahitaji ushindani.

Tangu kutolewa kwa maazimio yasioeleweka na na Benki Kuu Cyprus na kulazimisha kitengo cha huduma za kadi kuwa nje ya soko, Cyprus imerudi kenye ukiritimba.

Sasa ni nini tunakisikia? Kama ilivyotarajiwa, ada za JCC kwa wafanyabiashara zinapanda tena, na hii inachangia kongezeka kwa kwa ujumla kwa bei katika maduka, hoteli, migahawa nk.

Kupanda kwa bei, watu kupoteza ajira zao, na Kampuni kulazimishwa kusimamisha shughuli zake? Jibu ambalo si sahihi kabisa kwa uchumi uchumi unaoanguka!

Mengineyo

Cyprus ni lazima ifanye kila kitu linalowezekana kuwafanya watu wawe na kazi; kwa nini Benki Kuu ya Cyprus wanaachwa kuendelea kwa kosa hili?  Hakuna hata tamko moja kutoka duru rasmi za uongozi.