Wachunguzi Wapya Wa CBC Waingia FBME Tawi La Cyprus

Aprili 30, 2015

Benki Kuu ya Cyprus (CBC) imewateua wachunguzi wapya ili kukagua mifumo ya kupambana na fedha chafu kwenye tawi la FBME Cyprus. Washauri walioteuliwa na Benki Kuu ni kampuni ya sheria ya kimataifa ya DLA Piper, wachunguzi wa fedha Kroll na wanasheria wa Cyprus Georgiades & Pelides.

Benki ya FBME itatoa ushirikiano kamili kwao katika jitihada za kusafisha madai yaliyotolewa na Benki Kuu mwezi Julai mwaka jana.

Ni vigumu kupinga ukweli kwamba hatua hii ilitakiwa kuchukuliwa miezi tisa iliyopita. Madhara mengi kwa wateja wa FBME, makampuni mbalimbali, wafanyakazi na Benki yenyewe labda yangeweza kuepukwa. Zaidi ya hayo, gharama kubwa iliyosababishwa na CBC kwa niaba ya walipa kodi wa Cyprus ingeweza kwa kiasi kikubwa kupunguzwa.

Tangu Julai mwaka jana, FBME Limited, kwa niaba yake yenyewe, iliruhusu wachunguzi wa uhasibu wa kampuni ya sheria ya kimataifa Hogan Lovells na wataalamu wa mahesabu E & Y (Ernst and Young) USA. Matokeo ya uchunguzi huo yamewasilishwa kwenye Idara ya Hazina ya Marekani – FinCEN katika hatua kadhaa kati ya Septemba na Desemba mwaka jana. FBME imeomba maazimio ya FinCEN yaondolewe kwa misingi ya matokeo ya wataalamu wa Marekani na kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano kamili na mamlaka za Marekani.

Itakumbukwa kwamba Benki Kuu ya Cyprus ilifanya chunguzi tano tofauti katika suala hili hili zilizofanywa na wakaguzi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na PwC, kati ya majira ya joto na mwishoni mwa mwaka jana. Matokeo ya uchunguzi huo kamwe hayajawekwa hadharani na CBC. Hii ni pamoja na ukaguzi wa kawaida wa kila mwaka wa Benki Kuu unaofanywa na wakaguzi wa nje K Treppides and Co, na uchunguzi maalum uliofanyika mwaka 2013 na KPMG ya Ujerumani.

Benki Kuu sasa imemteua Andrew Andronikou, mtaalamu wa uhasibu wa UHY Hacker Young chartered yenye makao yake mjini London, kama Msimamizi Maalum Mwenza wa tawi la Benki ya FBME Cyprus kufuatia kuteuliwa kwa Dinos Christofides mapema mwezi Julai. Mr Andronikou ameanza uteuzi wake leo.