Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi ICC inaona inayo mamlaka Kusuluhisha Kesi kati ya Wamiliki wa Benki ya FBME na Jamhuri ya Cyprus

Septemba 16, 2015

 Kwenye maamuzi yake yaliyosainiwa tarehe 10 Septemba 2015, Mahakama ya Kimataifa ya Biashara (ICC) mjini Paris aliamua kwamba ina mamlaka juu ya madai ya wamiliki wa FBME Limited (Wadai) dhidi ya Jamhuri ya Cyprus (Washtakiwa) kuhusu Mkataba wa Lebanon-Cyprus unaosimamia ulinzi wa haki za mwekezaji.

Kwa hiyo pingamizi la washitakiwa la kudai kuwa mahakama ya usuluhishi inakosa mamlaka ya kusikiliza kesi yametupiliwa mbali na usuluhishi utaendelea na awamu yake ya pili. Katika kutoa maamuzi hayo, mahakama hiyo imeliondoa ombi la gharama za kesi kwenye awamu hii ya usuluhishi ambayo inashughulikia uhalali wa kesi kwa wadai, pamoja na tathmini ya uharibifu na fidia.

Tovuti hii itatoa taarifa zaidi juu ya mada hii na maendeleo mengine yanayotokana na kesi ya usuluhishi.

Wamiliki wakuu wa Benki ya FBME walifungua mashitaka kuomba usuluhishi Oktoba 28, 2014 wakitumia sheria ya mwaka 2003 ya ‘Makubaliano ya Kubadilishana, kutangaza na kutetea Uwekezaji kati ya Jamhuri ya Lebanon na Jamhuri ya Cyprus’. Ibara ya 6 ya Mkataba huu inakataza kutaifisha au kupoka mali za raia wa nchi hizi, wakati Ibara ya 12 inatoa ruhusa kwa usuluhishi miongoni mwa mambo mengine, kutatua migogoro.

Walichukua hatua hii kufuatia uamuzi wa Benkki Kuu ya Cyprus wa kuliendesha tawi ka Benki ya FBME tawi la Cyprus mnamo Julai 2014, kuanzishwa kwa hatua zisizo sahihi za Azimio na jaribio la kuuza tawi kinyume na matakwa yao, kama wamiliki.

Jamhuri ya Cyprus iliwasilisha majibu yake kwenye mahakama ya usuluhishi Januari mwaka huu, wakidai kwamba mahakama hiyo haina mamlaka kwa sababu tawi la Cyprus na wamiliki wake hawahusiki na mikataba huo. Mahakama ya Usuluhishi sasa imeikataa hoja hii na kuamua kwamba Mkataba baina ya nchi hizi upo.

Ikiwa jijini Paris, mahakama ya ICC ni chombo kinachoongoza ulimwenguni katika utatuzi wa migogoro ya kimataifa na usuluhishi. ICC ina shughuli kuu tatu: Kutunga sheria, Utatuzi wa migogoro, na Utetezi wa sera. Kwa sababu makampuni wanachama wake na vyama ni wenye kushiriki katika biashara ya kimataifa, ICC ina mamlaka makubwa katika sheria zinazoongoza na kusimamia uendeshaji wa biashara na mikataba nje ya mipaka ya nchi mbalimbali.

Katika utangulizi wa kitabu chake juu ya Sheria ya Usuluhishi, ICC inasema: “Usuluhishi chini ya Sheria ya ICC ni utaratibu rasmi unaopelekea uamuzi wa kisheria usiofungamana na upande wowote, unaohusika na utekelezaji kwa mujibu wa sheria za ndani za usuluhishi na mikataba ya kimataifa kama vile mikataba wa New York wa 1958.