FBME Yaja na Mpango Wa Kuwafungulia Milango Wateja Wake

Oktoba 31, 2015

 Benki ya FBME imeanzisha mipango ya kuhamisha amana zilizoko katika tawi la Cyprus kwenda kwenye ofisi za makao Makuu nchini Tanzania, ambapo kwa njia hii itawawezesha wateja wake kupata fedha zao. Hii inafuatia hali ambapo wateja wamekuwa na vikwazo vya kuchukua kiasi kidogo cha EUR 1,000 kwa wiki na wakati mwingine wamekuwa wakiwekewa Ukomo kwenye akaunti zao kwa amri ya Benki Kuu ya Cyprus (CBC), ambayo walichukua udhibiti wa FBME tawi la Cyprus mwezi Julai 2014.

FBME imeiandikia CBC ili kupata idhini ya mamlaka ya Cyprus kuhusiana na mpango huu. Barua ya kwanza alipelekwa tarehe 20 Oktoba na kufuatilia wiki hii iliyopita kupata majibu kutoka Benki Kuu. Bado hawajajibu maombi rasmi ya kuhamishia akaunti hizo kwenda Tanzania.

Hatua hii imefuatia mawasiliano kati ya Benki ya FBME na wengi wa wateja wake katika kutafuta njia mbadala ili wateja wapate kutumia fedha zao. Wakati huo huo inaipunguzia mamlaka hiyo ya Cyprus suluhishio la tatizo la ulipaji wa kiwango kamili cha bima ya ulinzi wa amana kwa fedha inayomilikiwa na tawi FBME la Cyprus.

Kwa kipindi cha miezi 15, FBME imejaribu mbinu nyingi ili kuwawezesha wateja wake kupata udhibiti wa fedha zao zilizopo kwenye tawi la Cyprus. Mbinu hizo ni pamoja na mazungumzo pamoja na ushirikiano na CBC, madai katika mahakama na usuluhishi kwenye mahakama ya kimataifa ya ICC mjini Paris. Bila kueleza sababu zake, CBC imekuwa ikizidharau mbinu hizo, wakati huo huo ikiingia kwenye madhara ya kihadhi, gharama kubwa kwa walipa kodiwa Cyprus na hatari kubwa zaidi ya kupoteza mamia ya mamilioni kwenye malipo ya fidia.

Matatizo yanatokana na uamuzi CBC wa kupoka tawi la FBME Cyprus mwezi Julai mwaka 2014, kwa kutumia azimio la amri ambalo halikuwa na misingi ya kisheria. Ilifungia upatikanaji wa huduma ya akaunti kwa wiki sita na kutaka kuuza tawi bila kuwashirikisha wamiliki wa benki au mameneja. Hatimaye CBC waliteua watendaji wa kuuza au kulifunga tawi bila kuelewa matokeo ya maamuzi yao haramu. Suala la kushangaza, mwanzoni kabisa CBC ilisema inachukua hatua hiyo ili kulinda maslahi ya wateja, suala ambalo ilishindikana kufuatia maamuzi yake ya baadae.

Kutekelezwa kwa hatua ya azimio la amri kwa FBME tawi la Cyprus kulifanywa bila kuwashirikisha mthibiti mkuu wa benki, Benki Kuu ya Tanzania, au wamiliki wake au mameneja.

Ilikuwa ni moja tu ya idadi ya maamuzi mabaya yaliyochukuliwa na CBC na mawakala wake kwenye sekta yote ya benki ambayo yalileta upinzani mkali kutoka ndani na nje ya nchi. Mengi ya haya yanatokana na kitengo cha Azimio cha CBC kilichoongozwa na Michalis Stylianou.

CBC na vyombo vyake vya azimio wamejiweka wenyewe kwenye kona na chaguo bora walilo nalo kwa sasa ni kuwaachia wateja wahamie Tanzania, kwa wale watakaochagua kufanya hivyo. FBME itaendelea kujitahidi kufanya kazi na mamlaka za Cyprus kutafuta ufumbuzi bora kwa ajili ya wateja.