FBME Yapambana na CBC Kisheria dhidi ya Ubatilishaji wa Leseni Yake

21 Desemba 2015

FBME Limited imetangaza kuwa hatua za haraka za kisheria zitachukuliwa kupinga kusitishwa kwa leseni, kulikofanywa na Benki Kuu ya Cyprus (CBC) dhidi ya Benki ya FBME Tawi la Cyprus, na uamuzi huu kwenye mahakama ya Cyprus.

Tamko la ubatilishaji huo lenye kurasa 9 limewasilishwa leo Desemba 21, 2015, ikilaumu watendaji wengine kwa vitendo vilivyosababishwa na hatua zilizochukuliwa na Bodi ya CBC katika kipindi cha miezi 17, ambayo imetokana na CBC ilipofanya jaribio la uuzaji wa Benki ya FBME ya tawi Cyprus. FBME inapinga kabisa kubatilishwa kwa leseni hiyo.

Hatua hii ya kidhalimu ya CBC dhidi ya FBME, ambayo ni ya hivi karibuni, imesababisha kesi mbili nchini Cyprus na nje ya nchi, na kuziacha mamlaka za Cypruskwenye mlolongo wa madai ya uharibifu mkubwa na fidia.