FBME Yaiumiza Vichwa CBC

Juni 16, 2015

Miezi kumi na moja baada ya uamuzi usiokuwa wa kawaida wa CBC wa kuchukuwa operesheni za FBME nchini Cyprus, wasiwasi wa umma unamiminika huku vyombo vya habari nchini vikionyesha kuwepo wasiwasi huo. Gazeti la kila wiki kisiwani Cyprus, linalochapishwa kwa Kiingereza limeandika makala ifuatayo:

“Wakati Benki Kuu ya Cyprus alipochukua uamuzi usiokuwa wa kawaida Julai 2014, kwanza kwa kusitisha, na kisha kujaribu kuuza shughuli za FBME Cyprus, tawi la benki yenye makao yake Tanzania, kufuatia madai ambayo hayajathibitishwa kuhusu fedha chafu, haikuweza kuona hatari inayoweza kutokea.

Mwishoni mwa mwezi uliopita, karibu mwaka baada ya uamuzi, na wakati Benki ikiwa chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Azimio, Mahakama ya Kimataifa ya Biashara ya (ICC) – ambapo kesi ya kufungwa kwa Benki ya FBME ilifunguliwa na wamiliki wake wakuu Ayoub-Farid Michel Saab na Fadi Michel Saab – waliitaka Jamhuri ya Cyprus kujiepusha na kuendelea kuuza au kufanya utatuzi kabla ya mwisho wa usuluhishi.

Mamlaka ya Azimio imetakiwa kujiepusha na kuchukua hatua yoyote ambayo ingeweza kuharibu biashara ya FBME Cyprus hadi kukamilika kwa usuluhishi, na walitakiwa kutoa taarifa – mwezi mmoja mapema – kwenye mahakama hiyo, Wadai, Wakili wao na Msimamizi Mkuu wa Benki aliyeteuliwa na Benki Kuu ya Tanzania, kwa maamuzi yeyote waliotaka kuyachukua.

Mahakama hiyo ya usuluhishi imepuuza maombi kadhaa na wadai, ikiwa ni pamoja na uharibifu uliotokea, kwa msingi kwamba kuamua hayo kutahatarisha uhalali wa kesi. Mahakama ya usuluhishi inatarajiwa kutathmini mwenendo wa Jamhuri ya Cyprus katika hatua ya baadaye, wakati itakapoamua juu ya uhalali wa mgogoro na ukubwa wa fidia, matarajio ambayo yamezua ‘kengele ya tahadhari’ kwa Benki Kuu na wizara ya Fedha, kwa mujibu wa ripoti ya vyombo vya habari.

Mapema mwaka huu ujumbe wa wawakilishi wa Benki ya FBME wameripotiwa kuwa walikutana mjini Washington DC Marekani na Idara ya Hazina ya FinCEN na kujibu madai ya fedha haramu. Benki ya FBME iliwasilisha mamia ya kurasa za nyaraka kutokana na uchunguzi wa kina uliofanywa na Ernst and Young na kampuni ya sheria Hogan Lovells. FBME ilisisitiza kuwa inabakia na nia ya kuendelea kushirikiana na Marekani, Cyprus na serikali ya Tanzania.

Vyanzo vya karibu na kesi vinasema kwamba wiki tu kabla ya Ilani ya FinCEN Benki Kuu ya Cyprus ilifanya ukaguzi wake wa mara kwa mara. Vyanzo hivyohivyo vinaonyesha ukweli kwamba hakuna ripoti ya uchunguzi huu iliyotolewa na hivyo kuchochea utambi kwa uvumi kuhusu nia ya uchunguzi uliofanywa baadae kwa FBME. Pia imezusha maswali kuhusu jinsi Benki Kuu ilivyokuwa ilitoa majibu yake wakati kukiwa na madai ya kuyumba kwa sekta ya Benki ya Cyprus na wakati huo washindani walikuwa wakitaka kurudi kwenye soko.

 Hivi karibuni Mamlaka ya Azimio ilimteua Andrew Andronikou kama Msimamizi Maalum kuchukua nafasi ya Dinos Christophides ambaye alijiuzulu katika mazingira ya kutatanisha. Uteuzi wa Mheshimiwa Andronikou, umeelezwa na vyanzo vya karibu na kesi kama “Usio wa kawaida” kutokana na kwamba ana uzoefu mkubwa katika Kuuza na kufilisi Makampuni – matarajio ambayo ICC inakataza – ila ana uzoefu kidogo sana katika kuendesha Benki iliyo chini ya Azimio.

Benki ya FBME ni moja ya benki kubwa za kibiashara nchini Tanzania, ikiwa na jumla ya mali zenye thamani ya takriban Dola za Marekani Bilioni 2.72, na mali ya wanahisa ya takriban Dola za Marekani Milioni 179, na ina ofisi jijini Dar es Salaam, Nicosia, Limassol na Moscow. “

Kwa nakala halisi ya makala, bofya hapa.