Mahakama ya Wilaya ya yapuuza ufunguaji wa kesi Usuluhishi ya FBME

Desemba 19, 2014

Jana, tarehe 18 Desemba 2014, Benki Kuu ya Cyprus ilitoa taarifa zenye kauli za kiholela na zisizo sahihi kuhusu uamuzi wa Mahakama ya Wilaya uliofanywa tarehe 17 Desemba.

Ingawa Mahakama ya Wilaya ya Nicosia imekataa maombi yaliowasilishwa na wanahisa wa FBME Bank kuzuia uuzaji wa tawi la Benki ya Cyprus, kunakuwa hakuna tofauti kwa maana usuluhishi utaendelea kusikilizwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Biashara katika mji wa Paris itaendelea kama ilivyopangwa. Zaidi ya hayo, wanahisa wa FBME, tarehe Desemba 22 watakata rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama ya Wilaya ya Mahakama Kuu na vile vile itaendelea kutafuta fursa nyingine za kisheria.

Wakati huohuo hatua yoyote itakayo chukuliwa na Mamlaka ya Azimio kwa aijili ya kuuza tawi la Cyprus. FBME Benk itafanya juhudi zote za kisheria zilizopo kuzuia. Mtu yeyote ambaye atajihusisha katika mchakato huo, ikiwa ni pamoja na wale ambao wanaingia katika mazungumzo na Mamlaka za Benki Kuu ya Cyprus, atakuwa amehusika.

Uamuzi huu wa mahakama hauleti hasara wala hata kuturudisha nyuma. Yote yaliyotokea ni kwamba Mahakama ya Wilaya iliamua kwamba haitaweza kuruhusu maombi ya mpito ya FBME kusitisha uuzaji wakati usuluhishi ni unaendelea katika Paris.

Ni muhimu kuweka wazi kwamba Mahakama ya Wilaya Cyprus haiwezi kuwa ilitoa tawala juu ya uwekezaji wa wamiliki wa FBME, Ayoub-Farid M Saab na Fadi M Saab, chini ya mkataba wa Lebanon-Cyprus.  Mkataba ya aina hii inasikilizwa katika  Mahakama katika ICC mjini Paris. Muundo wa umilikaji wa FBME Bank unajulikana Benki Kuu ya Cyprus, ambayo ni Benki msimamizi kwa miaka 32 sasa.

Ukweli unabaki kuwa Wahojiwa (Jamhuri ya Cyprus) wameteua msikilizaji wao kwa ajili ya kesi ya usuluhishi ICC, pamoja na msuluhishi aliyeteuliwa kuna mchakato wa kuteua Rais wa Mahakama. Katika wiki chache zijazo, Mahakama itaundwa kama mfumo wa mahakama ambayo ina mamlaka ya kipekee ya kuamua hadhi ya ‘wawekezaji’.

Wanahisa wa FBME Bank wanaendelea kusisitiza kuwa ni imani yao mahakama ya usuluhishi ICC litaangalia suala hili kitaalaam zaidi wakiwa huru na kutunza heshima za utawala wa sheria za kimataifa.

Madai yaliyotolewa na Benki Kuu ya Cyprus katika taarifa yake ya 18 Desemba si ya kweli na hayana mazingatio. Inaonekana kama sehemu ya uadui dhidi ya FBME Bank.

Itakumbukwa kwamba tangu mwanzo wa jambo hili tarehe 21 Julai 2014, si Benki Kuu ya Cyprus wala msimamizi wake kwa wakati wowote walitaka ushauri FBME Bank, wamiliki wake au mdhibiti wake wa nyumbani, Benki Kuu ya Tanzania, juu ya mapendekezo ya kuuza tawi la Cyprus.