Maamuzi ya Kutapatapa huku CBC Ikielekea kukwama

Machi 13, 2015

 Pamoja na kukabiliwa na matatizo lukuji waliojisababishia wenyewe Benki Kuu ya Cyprus (CBC) inajitutumua na maamuzi mabovu zaidi na kuthibitisha kuwa wao bado ni chombo hatari wakati Gavana na Wakurugenzi Waandamizi wa CBC, (mmoja amejiuzulu jana) wanakabiliwa na maswali toka kwa wabunge na pia matatizo la malipo ya fidia yakiendelea kukua siku hadi siku, CBC inajali tu kuendeleza upuuzi wake.

Sasa, baada ya karibu miezi minane ya maamuzi yake yote kuhusu kuuza tawi la FBME kutozaa matunda, kuna mapendekezo kwamba CBC inaazimia kufunga leseni ya kuendesha tawi, matokeo yake yatarudisha udhibiti wa Benki kwenye Ofisi yake Kuu iliyopo nchini Tanzania.

Kama ambavyo tumeonesha mara kadhaa kwenye tovuti hii, Benki ya FBME bado ipo kwenye nafasi nzuri kiukwasi, ikiwa na uwezo wa kukidhi mahitaji yote ya wateja wake mara baada ya kesi yake kuhusiana na tawi la Cyprus itakapoamuliwa na Mahakama ya Usulihishi ya Kimataifa ya Biashara jijini Paris.