Maoni kutoka Kwa Profesa wa Chuo Kikuu cha Columbia

Februari 10, 2016

Maoni zaidi kwenye tovuti ya FinCEN kuhusu jinsi idara hiyo inavyoshughulikia kesi ya FBME, yamewasilishwa na Sharyn O’Halloran, Profesa wa George Blumenthal katika Chuo Kikuu cha Columbia jijini New York. Katika barua yake iliyotumwa kwa FinCEN na kuwekwa kwenye tuvuti ya umma, Profesa O’Halloran alieleza kuwa eneo lake la kitaalamu ni utafiti wa michakato ya utawala ya Marekani, mamlaka ya kisheria na majukumu ya usimamizi.

 

“Idara kama FinCEN ina utaalamu mkubwa katika uhalifu wa ‘Kola Nyeupe’ ndani na nje ya nchi, na hivyo ni lazima wawe na urasimu kwa kiasi flani” aliandika. “Hata hivyo, mamlaka hii maalum haipaswi kuiingiza idara kutekeleza malengo yake binafsi kinyume na maslahi ya umma.

“Masuala fulani ya kesi hii yanaonyesha idara hii inatekeleza ajenda zake yenyewe, badala ya mamlaka waliyopewa na Bunge. Kutoka kwenye kesi za mahakamani na maoni ya umma, ni dhahiri kwamba FinCEN imekiuka Sheria ya Utaratibu (APA) katika kuamua hatma dhidi ya FBME. Mbaya zaidi, inaonekana kwamba matendo kadhaa ya FinCEN dhidi ya FBME yanafanywa kinyume na utaratibu wa kikatiba. ”

Ili kuzuia hili kutotokea mara kwa mara anatoa wito kutungwa kwa taratibu za udhibiti zenye nguvu “… ili kuzuia ukiukwaji dhidi ya taasisi nyingine za fedha”

Profesa O’Halloran aliongeza kuwa FinCEN imeonyesha uzembe katika kutathmini ushahidi uliotolewa na kwenye kutoa taarifa kwa FBME, huu ni ukiukwaji wa Sheria ya Utaratibu (APA). “FinCEN inaonekana kutozipa uzito hatua zilizochukuliwa na FBME katika kurekebisha na kuboresha udhibiti wake wa ndani. FinCEN pia inaonekana kupuuza matokeo ya wakaguzi huru Ernst and Young na KPMG kwamba benki ilikuwa inakidhi viwango vya kimataifa na vya ndani vya kudhibiti fedha chafu (AML). Aidha, Idara hiyo ilitoa kauli potofu kuhusu muda na ukubwa wa faini za zamani zilizowekewa FBME.

“Idara yenge nguvu kubwa ya kimaamuzi haiwezi kumudu kufanya makosa ya kizembe. Katika kutekeleza mamlaka yake ya kimaamuzi, FinCEN inatakiwa kufikia viwango vya kiushahidi na kukanusha taarifa isizokubaliana nazo. Haiwezi tu kupuuza, kushindwa kufichua au kushabikia taarifa za uongo. ”

Aliongeza, “Wakati wa kutoa hukumu nzito, kama ya kukataza shughuli za msingi za kibenki zinazoruhusiwa chini ya kifungu cha 311 cha Sheria ya Ndani ya Marekani, FinCEN lazima watengeneze na kutekeleza taratibu za maamuzi zenye uwazi na uwajibikaji ambazo zinakidhi na kuzingatia viwango vya udhibiti wakati wa kutathmini mabenki”.

Kupata Maoni ya Profesa O’Halloran nenda kwenye tuvuti: http://www.regulations.gov/#!docketBrowser;rpp=25;po=0;dct=PS;D=FINCEN-2014-0007;refD=FINCEN-2014-0007-0057