Tahadhari ya Uzzaji wa Mali

Juni 25, 2016

FBME Limited, kampuni ya tanzu ya Benki ya FBME (“Benki”), imegundua kwamba Msimamizi Maalum aliyeteuliwa na Benki Kuu ya Cyprus (CBC) anajaribu kuuza mali ambazo ni mali ya Benki. Jitihada za kuuza mali za Benki zinafanyika bila taarifa au ridhaa ya Meneja wa Kisheria wa Benki Kuu ta Tanzania ambaye ndio mdhibiti mkuu.

Aidha, vitendo hivi vya Msimamizi Maalum vinatendeka wakati ambapo Mahakama Kuu ya Cyprus bado haijatoa hukumu juu ya maombi ya CBC ya kuifilisi Benki. Kwa kifupi, Msimamizi Maalum hana uwezo wa kisheria wa kuuza mali za Benki na kwa hiyo mali hizo hazitakuwa halali kwa wanunuzi watarajiwa.

 

Ili kulinda haki za Benki, wateja na wamiliki wake, uhamisho wowote unaotegemewa kufanywa wa mali za Benki utatakiwa ufuate taratibu za kisheria ipasavyo ili kuziweka huru kwa ajili ya kuuzwa na wanunuzi watarajiwa wa mali hizo wanapewa tahadhari hiyo.