Yaliyojiri kuhusu Usuluhishi

Desemba 13, 2014

Jamhuri ya Cyprus ilitakiwa kuwasilisha majibu kwenye mahakama ya usuluhishi ya ICC tarehe 5 Desemba kwenye shauri lililofunguliwa na wamiliki wa Benki ya FBME. Jamhuri iliomba muda wa ziada wa kujibu, ambao umetolewa, na tarehe mpya ni 7 Januari.

Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi ICC yenye makao yake jijini Paris ilianzishwa mwaka 1923 na kuongoza maendeleo ya usuluhishi wa kimataifa wa kibiashara kama inavyojulikana leo. Mahakama hutoa msimamo wa kati kwa wanaoshitakiana kwa ajili ya utatuzi wa migogoro na maamuzi yake yanatambuliwa kimataifa, takribani nchi 145, ikiwa ni pamoja na Cyprus, zimesaini Mkataba wa New York mwaka 1958 unaoitwa ‘Tuzo ya Utambuzi na Utekelezaji wa Mambo ya Nje ya Usuluhishi’. Tangu kuanzishwa kwake, Mahakama imesuluhisha kesi zaidi ya 20,000.

ICC – International Chamber of Commerce – iliundwa jijini Paris mwaka 1919 na ni shirika kubwa na lenye uwakilishi mkubwa wa kibiashara duniani. Kupitia mamia ya maelfu ya wanachama, lina mamlaka ya kuaminika katika kutengeneza sheria zinazotawala mwenendo wa uendeshaji biashara kuvuka mipaka ya nchi mbalimbali.

Wanahisa wa FBME walileta shauri kwa usuluhishi kwenye mahakama ya ICC dhidi ya Jamhuri ya Cyprus tarehe 28 Oktoba kwa mujibu wa Makubaliano ya Ulinzi wa Uwekezaji kati ya Lebanon na Cyprus ya tarehe 9 Aprili 2001. Hii ni kuhusiana na uchukuaji wa tawi la Cyprus la Benki ya FBME kulikofanywa na Benki Kuu ya Cyprus na jitihada zake za kutaka kuliuza tawi lililokuwa na fedha za kutosha.

Wanahisa waliomba uteuzi wa jopo la mahakma ili kutatua mgogoro mara moja kabla ya madhara zaidi yaliyosababishwa na Benki Kuu ya Cyprus. Wanahisa hao wanadai fidia kwa madhara yaliyosababishwa na vitendo vibaya vya Benki Kuu ya Cyprus yanayokadiriwa kufikia Dola za Kimarekani Milioni 500.