Agizo la Kwanza Latolewa na Mahakama ya Usuluhishi

Februari 21, 2015

Tarehe 20 Februari 2015, Mahakama ya Usuluhishi ya ICC mjini Paris ilitoa maamuzi yake ya kwanza, yanayojulikana kiutaratibu kama “Agizo 1 au Order No 1.’ Maneno yaliyomo kwenye agizo hilo ni kama yafuatayo:

” Mahakama ya Usuluhishi inamtaka mshitakiwa kutoendelea kuuza kama utatuzi wa Benki ya FBME na kutohamisha fedha zake kwenda Benki Kuu ya Cyprus kabla ya maamuzi ya Mahakama ya Usuluhishi yaliyowasilioshwa na Wadai.”

Wadai ni wamiliki halali wa Benki ya FBME na Jamhuri ya Cyprus inawakilisha Mshitakiwa. Agizo lisilo na mashaka  linahusu zuio la muda kwa hatua zozote zinazoweza kuchukuliwa na Benki Kuu ya Cyprus, kama Mamlaka ya Kiutendaji,  na Msimamizi Maalum, dhidi ya Benki ya FBME tawi la Cyprus wakati Mahakama inaendelea na kesi hii.

Ni vema tukajikumbusha historia fupi ya sakata la Mahakama ya Usuluhishi:

Tarehe 21 Julai 2014 Kamati ya Azimio, iliyopewa madaraka na Mamlaka ya Azimio, alitangaza nia yake ya kuuza tawi la Benki ya FBME la Cyprus. Kwa mujibu wa ‘Makubaliano ya Kubadilishana Ulinzi wa Uwekezaji ‘kati ya Jamhuri ya Cyprus na Jamhuri ya Lebanon, tarehe 9 Aprili 2001, wanahisa wa Benki ya FBME walipeleka ombi kwenye Mahakama ya usuluhishi ya Biashara ya Kimataifa (ICC) iliyopo mjini Paris. Shauri hili lilifunguliwa tarehe 28 Oktoba 2014.

Wanahisa waliiomba Mahakama kutatua mgogoro kabla ya madhara yasiyoepukika kusababishiwa tawi la FBME la Cyprus na Benki Kuu ya Cyprus, Mamlaka ya Azimio na Msimamizi Maalum. Wanahisa wanadai fidia kwa uharibifu wa Dola za Kimarekani Milioni 500.

Shauri hili linaendeshwa na jopo la watu watatu ambao ni Professor Puierre Tercier (Mwenyekiti) na washirika wake Profesa Ibrahim Fadlallah na VV Veeder QC.

ICC ni Shirikisho Kubwa duniani kwenye masuala ya biashara. Ina shughuli kuu tatu: kuweka sharia za utawala, utatuzi wa migogoro, na utetezi wa sera. Kwa sababu wanachama wake ni makampuni na vyama wanaojishughulisha na bishara za kimataifa, ICC ina mamlaka makubwa katika kuunda sheria zinazotawala na kudhibiti uendeshaji wa biashara na mikataba kwenye nchi nyingi.